Home Kitaifa MIFUKO 250 YA SARUJI YA MBUNGE MUHONGO KUANZISHA UJENZI SEKONDARI MPYA YA...

MIFUKO 250 YA SARUJI YA MBUNGE MUHONGO KUANZISHA UJENZI SEKONDARI MPYA YA PROF. MASAMBA

Na Shomari Binda-Musoma

MIFUKO 250 ya saruji iliyochangwa na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo imeanzisha ujenzi wa shule mpya ya sekondari.

Saruji hizo zilipatikana kwenye harambee ya ujenzi wa shule hiyo ya kumbukumbu ya gwiji wa kiswahili hayati Profesa David Masamba.

Licha ya mchango huo wa Profesa Muhongo wadau mbalimbali pia walichangia na kupatika saruji mifuko 481, ikiwemo 50 ya familia ya Prof.Masamba

Pia mchanga lori 45 na mawe lori 31 fedha tasim shilingi 615,000 zikiwemo 500,000 zilizotolewa na familia ya Profesa Masamba.

Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uamuzi wa kuenzi kazi na mafanikio makubwa ya utaalamu na ubingwa mkubwa wa lugha ya kiswahili wa hayati Prof David Massamba ulifanywa na waombolezaji wote wakati wa mazishi yake.

Amesema kiiwanja cha uhakika na kikubwa kimepatikana kwenye Kitongoji cha Kati Kijijini Kurwaki

Muhongo amesema michoro ya majengo imetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Musoma huku eneo la ujenzi lkiwa limekidhi vigezo vyote hitajika.

Wadau mbalimbali wameombwa kuendelea kuchangia ujenzi wa shule hiyo inayojengwav Kitongoji cha Kurwaki kupitia akaunti ya serikali ya Kijiji cha Kurwaki benki ya NMB namba 30302301539

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!