VIJANA watakiwa kujikita katika nguvu kazi ya mikono yao kupata vipato vya halali ili kuepuka uhalifu na uharamia unaosababisha majanga kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Akizungumza Mpishi wa keki Alexander vitalis mara baada ya kufungua zoezi la uonjaji keki wa ladha mbalimbali ikiwa ni njia mojawapo ya kukutana na wateja wake na kutambulisha aina tofauti tofauti za keki zinazopatikana katika ofisi yake iliyopo Msasani jijini Dar es salaam amesema vijana ni muhimu kufanya kazi kwa bidii na kuweka mbele vipawa vyao ili kujikwamua kiuchumi na kujiepusha vitendo vya uhalifu kwani kumekuwepo na changamoto kubwa kwa vijana kukosa ajira na kutegemea kuajiriwa badala ya kutumia vipaji vyao kujiajiri.
“Takribani miaka 4 sasa nimekuwa Mpishi mzuri wa keki nje na ndani ya Tanzania na nimeajiri zaidi ya wafanyakazi 20 hivyo nimepiga hatua kubwa sana kuona kwa jinsi gani nawapa vijana wenzangu ajira Kupitia upishi wa keki hivyo naendelea kuwasisitiza vijana wenzangu hakuna kuchagua kazi hii ya jinsia fulani ni vyema wafanye kazi Ili wajiepushe na uhalifu kukosa ajira sio sababu ya kujiingiza na uhalifu”.
Hata hivyo vitalis amefafanua zaidi kuwa shughuli hiyo ya uonjaji keki utadumu kwa siku tatu ili waliombali waweze kusogea karibu kujua ladha tofauti tofauti za mapishi ya keki zinazopatikana katika ofisi yake huku wenye matatizo binafsi akiwa amewazingatia zaidi.
“Tunatengeneza keki za mchaichai,matunda,viungo na vitu mbalimbali ambayo kimsingi hata mwenye mzio(Allergy) anaweza kupata huduma ya keki bila tatizo, watu wenye visukari pia keki zao zipo wakaribie kupata huduma ya kuonja keki washerehekee miaka 4 ya huduma zetu za keki .”