Na Dickson Mnzava, Same.
Mbunge wa Jimbo la Same mashariki Mkoani Kilimanjaro Anne kilango Malecela amezindua shina la umoja wa vijana UVCCM Katika kijiji cha kadando Kata ya Maore jimbo la Same mashariki wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na vijana hao wakati wa uzinduzi huo mheshimiwa Anne kilango amewasihi vijana kuendelea kufanya kazi kwaumoja sambamba na kudumisha umoja na mshikamano ili kulinda heshma ya Chama cha mapinduzi pamoja kuyasemea mafanikio ya serikali kwa wananchi.
Amesema kundi la vijana ni nyenzo muhimu katika maendeleo ya Nchi hivyo ni vyema vijana wakaenelea kukaa katika umoja na kulinda amani iliyopo huku akiwaasa vijana kuepukana na makundi chonganishi yenye nia mbaya na taifa.
“Kwanza kabisa vijana kiukweli leo mmefanya jambo kubwa sana hata Mheshimiwa Rais wetu akiona hili jambo atafarijika sana maana nyie vijana ndio nguzo muhimu sana katika Taifa jambo hili mlilolifanya mmekiheshimisha Chama cha mapinduzi na hata mimi pia mmenipa faraja kubwa mno hakika juhudi zenu hizi nitaendelea kuziunga mkono kwa Asilimia mia moja na niwasihi endeleeni kuwaleta vijana wengine wote kwenye umoja wenu huu”.
“Alisema mheshimiwa Anne kilango”.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa shina hilo mwenyekiti wa UVCCM tawi la kadando Hosseni Mussa amesema wao kama umoja wa vijana UVCCM wamefanikiwa kuondoa makundi yote ya vijana na vijana wote waliopo kwenye tawi hilo ni makada wa Chama cha mapinduzi huku vijana hao wakimpongeza mbunge wa Jimbo hilo kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya kwa manufaa ya wananchi wa Jimbo hilo.
Hata hivyo katika uzinduzi huo mheshimiwa Anne kilango Malecela amechangia shilingi laki tano kwaajil ya miradi ya maendeleo kwenye mfuko wa umoja wa vijana hao.