Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Zungu amefungua semina ya wabunge kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).
Semina hiyo ina lengo la kueleza utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara katika mwaka wa fedha 2019/20 hadi 2023/24.
Akifungua semina hiyo Mei 20, 2024, Mhe. Zungu amesema Bunge linatambua namna TBS inavyopambana kuhakikisha ubora wa bidhaa unazingatiwa na BRELA imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Naye, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, amelishukuru Bunge kwa kuendelea kuisimamia wizara na taasisi zake kwenye utekelezaji wa majukumu yake.