Home Biashara MHE.TSERE AWAPONGEZA WAKULIMA WA WILAYA YA LUDEWA

MHE.TSERE AWAPONGEZA WAKULIMA WA WILAYA YA LUDEWA

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe.Andrea Tsere, amewapongeza wakulima wote wa Wilaya ya Ludewa waliopo kwenye maoneshe ya nanenane Jijini Mbeya kwa Upendo mkubwa waliouonesha kwa Wananchi wanaofika kutazama fursa mbalimbali kwenye banda la Wilaya hiyo kwa kuwapa wananchi elimu ya kilimo na parachichi bure.

Kauli hiyo ameitoa leo Agosti 4,2020 katika Banda la Halmashauri hiyo kwenye maonesho ya Wakulima Nanenane aliposhuhudia Wananchi wakishukuru wakulima hao mara baada ya kupatiwa elimu ya Kilimo bora cha parachichi na kupewa parachichi la kula.

Wananchi waliotembelea banda hilo wametoa hisia zao kwakusema kuwa, Maonesho ya nanenane ya Mwaka huu 2022 katika Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ni tofauti na miaka mingine kwa mpangilio mzuri wa mazao yao huku wakienda mbali zaidi kwakusema kuwa, Ludewa imeleta mazao na kutupatia elimu ya mazao yote lakini bado wakaona umuhimu wakutupatia na matunda bure hili ni jambo la kuigwa.

Mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Elvila amesema kuwa “Tumepata elimu ya Kilimo Cha bustani za mbogamboga nyumbani kwetu lakini pia wataalamu hawa wametupatia na mbegu za mbogamboga na kutushauri namna bora ya kuzipika mboga hizo hivyo niwapongeze sana wataalamu kutoka Ludewa” amesema Elvila.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!