Home Kitaifa MHE. MWINJUMA ATETA NA BALOZI WA ITALY DODOMA

MHE. MWINJUMA ATETA NA BALOZI WA ITALY DODOMA

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Hamis Mwinjuma (mwanafa) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italy nchini, Mhe. Giuseppe Sean Coppola katika ofisini za Wizara Mtumba jijini Dodoma, leo Agosti 29 2024.

Katika Kikao hicho wamejadili kuhusu ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Italy katika Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni, Boniface Kadili, watendaji wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!