Home Kitaifa MHE. MCHENGERWA AMEWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA DARAJA LA BIBI TITI

MHE. MCHENGERWA AMEWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA DARAJA LA BIBI TITI

Mwandishi wetu, Rufiji

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja la Bibi Titi Mohamed Mohoro Rufiji.

Daraja hilo hadi kukamilika linatarajia kugharimu sh.Biln 11.5 na litajengwa kwa miezi 18 likiwa na urefu wa mita 80.

Akizungumza katika hafla hiyo ambayo ilitanguliwa na utiaji wa saini mkataba wa ujenzi wa daraja hilo kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) na Mkandarasi ameishukuru Serikali kwa kukubalj kuidhinisha fedha za mradi huo.

Amesema daraja hilo litawaondolea kero wnafunzi waliokuwa wanakwama kuhudhuria masomo wakati wa mvua lakini pia wafanyabishara ambao walikuwa wanakwama kusafirisha bidhaa zao kipindi cha mvua.

Kadhalika Mchengerwa amesema ujenzi wa daraja hilo ni moja ya kitu ambacho kitainua uchumi wa wananchi wa maeneo hayo na kuondoa vifo ambavyo vilikuwa vinachangiwa na ukosefu wa kivuko cha uhakika kwenda upande wa pili.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kunenge amesema katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan mkoa huo umepokea sh. Trilion 1.19 za miradi ya Maendeleo kati ya hizo sh. Biln 102.1 ni za Miundombinu ya barabara kwa Wakala wa Barabara Tanroads na Tarura.

Ameeleza kwamba kati ya fedha za miundombinu fedha za Tarura ni sh. Biln 49.3 na kwamba kitendo cha Serikali kutoa zaidi ya sh. Biln 11 ujenzi wa daraja hilo unakwenda kufungua uchumi katika eneo hilo ambalo limekuwa kikwazo cha usafiri hususani kipindi cha mvua.

Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff amesema daraja hilo ambalo litajengwa kwa fedha za ndani likikamilika litadumu kwa miaka 100 litakuwa na makaravati mawili na barabara unganishi zenye urefu wa Km moja.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!