Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 18, 2024 ameelekea nchini uganda ambapo anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) ulioanza tarehe 15 – 20 Januari, 2024 na Mkutano wa Tatu wa Kusini wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+China utakaofanyika tarehe 21-22 Januari, 2024, Kampala – Uganda.