Home Biashara MHE. KIGAHE: LENGO LA SERIKALI NI KUONA WAFANYABIASHARA WANAFANYA SHUGHULI ZAO KATIKA...

MHE. KIGAHE: LENGO LA SERIKALI NI KUONA WAFANYABIASHARA WANAFANYA SHUGHULI ZAO KATIKA MAZINGIRA RAFIKI

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Exaudi Kigahe(Mb) amesema kuwa lengo la Serikali ni kuona wafanyabiashara wanafanya shughuli zao katika mazingira rafiki ili kuweza kunufaika na biashara zao.

Mhe. Kigahe amesema hayo Desemba 19, 2023 wakati wa ziara yake katika mpaka wa wa Kasumulu wa nchi ya Tanzania na Malawi uliopo wilayani Kyela.

Vilevile Mhe.Naibu Waziri amebainisha lengo la ziara hiyo ni kuona shughuli zinazofanywa kuwasaidia Wafanyabiashara na kuona Changamoto za Wafanyabiashara ili kama Serikali iweze kuzitatua na kusiwepo na vikwazo vyovyote vya kuwakwamisha na kuboresha Biashara za mipakani.

Vilevile Mhe.Kigahe amesema ujenzi wa kituo cha pamoja katika Mpaka huo umesaidia kupunguza muda mrefu uliokuwa unatumika kwa wafanyabiashara kuhudumiwa na vile vile kama Serikali inaangalia namna ya kujenga masoko ambayo yatadhibiti njia za panya ambazo wafanyabiashara wanatumia kutorosha na kuingiza magendo Nchini.

Aidha ametoa rai kwa watumishi wa Mpaka huo kutimiza wajibu wao kwa wakati na weledi ili kuwahudumia wateja ndani ya muda mfupi.

Kwa upande wa Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato wa Mpaka wa Kasumulo Bw. Leonard Mapunda amesema kuwa kama mamlaka wanaendelea kuweka mazingira rafiki ya ukusanyaji wa mapato kwa wafanyabiashara pamoja na kuwa karibu nao kwa kuwapa elimu kabla ya kulipa kodi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!