Home Kitaifa MHE. KIGAHE AWATAKA WMA KUFANYA UKAGUZI WA MIZANI MARA KWA MARA ILI...

MHE. KIGAHE AWATAKA WMA KUFANYA UKAGUZI WA MIZANI MARA KWA MARA ILI KUEPUSHA MIGOGORO YA VIPIMO SAHIHI

Naibu waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amewataka wakala wa Vipimo Mkoani Mtwara kukagua Mizani yote ambayo itatumika katika mauzo ya korosho kwa msimu huu unaoatarajia kuanza mwaka huu.

Mhe. Kigahe ametoa maagizo hayo tarehe 10 Septemba, 2022 alipotembelea na kufanya ukaguzi katika Ofisi ya Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Mtwara na kusema kuwa ukaguzi huo wa Mizani kufanyika mapema na mara kwa mara utasaidia wakulima pamoja na wafanyabiashara wote kunufaika na zao la korosho na kupunguza migogoro ya ujazo au Vipimo sahihi.

Mtwara ndiyo kitovu cha biashara ya korosho na uchumi wa nchi hii Kama tunavyojua trillioni nyingi za fedha zinatokana na mauzo ya korosho Sasa tusingependa kuona Mtwara inakuwa nyuma kunufaika na zao hilo na moja ya njia ya kuhakikisha Mtwara inanufaika ni kuhakikisha mizani inakaguliwa mara kwa mara hasa msimu huu unaokuja wa mauzo ya korosho” Amesema, Mhe. Kigahe.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed Amesema kuwa Mtwara ni kitovu Cha Biashara na uchumi wake unakuwa Kwa Kasi zaidi.

Mhe. Kanali Ahmed amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo miradi ya miundombinu ya barabara, zahanati, shule pamoja na kuishughulikia ujenzi wa Viwanda vya kuchakata malighafi za Kilimo, Viwanda vya Saruji, Sabuni na sukari.

Mhe. Kanali Ahmed amesema kuwa WMA ina jukumu kubwa la kuhakikisha inakagua na kuisimamia Vipimo sahihi vya Mizani yote ya magari, mitungi ya gesi, dira za maji na mafuta.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa WMA Bw. Deogratius Maneno Amesema kuwa WMA ina jukumu kubwa la uhakiki wa Mizani, dira za maji na gesi, kutoa ushauri wa kitaalamu wa Vipimo na kufanya kaguzi za Mizani na Vipimo.

Mhe. Kigahe katika ziara yake Mkoani Mtwara ameambatana na Viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Hashil Abdallah na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mjini Mhe. Dunstan Kyobya.

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!