Home Kitaifa MGORE AWAHUSIA MAADILI MAZURI VIJANA WA CCM MUSOMA MJINI

MGORE AWAHUSIA MAADILI MAZURI VIJANA WA CCM MUSOMA MJINI

Na Shomari Binda-Musoma

MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji Taifa ya Jumuiya ya Wazazi Mgore Miraji amewahusia vijana was Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Musoma mjini kuwa na maadili mazuri na kuheshimu viongozi.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifunga kambi ya mafunzo ya vijana hao ya kuwajenga kimaadili na elimu ya ujasiliamali yaliyoandaliwa na Chama cha Mapinduzi wilaya ya Musoma mjini.

Amesema mafunzo waliyoyapata walipokuwa kambini ni muhimu na yanapaswa kuzingatiwa na kila mmoja.

Mgore amesema vijana ndio tegemeo ndani ya chama hivyo kupata mafunzo yakiwemo ya maadili yatawafanya kuwa vijana wazuri.

Amesema suala la maadili ni jambo zuri vijana kufundishwa ili chama kiweze kupata viongozi bora wa baadae.

“Nawapongeza kwa kumaliza mafunzo yenu ya kambi iliyofanyika hapa chuo cha maendeleo ya jamii Buhare”

“Naamini mtakuwa mmejifunza mengi ikiwa ni pamoja na kuwa na maadili mazuri hivyo naamini mtazingatia yale yote mliyofundishwa” amesema Mgore.

Mgore ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Wazazi Taifa kutoka mkoa wa Mara amewataka vijana hao kuitumia elimu ya ujasiliamali waliyoipata kuitumia vizuri katika kujiwezesha kiuchumi.

Baadhi ya vijana walioshiriki kambi hiyo wamewashukuru viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Musoma mjini kwa kuwaandalia kambi na kuwapa elimu.

Pia vijana hao pia wamemshukuru mbunge wa jimbo la Musoma mjini,Vedastus Mathayo,kwa kuwapa elimu ya ujasiliamali ambayo imewasaidia kuwajengea uwezo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!