Home Kitaifa MGORE AFANIKISHA KUPATIKANA BAJAJI MRADI WENYEVITI WA MITAA

MGORE AFANIKISHA KUPATIKANA BAJAJI MRADI WENYEVITI WA MITAA

Na Shomari Binda-Musoma

MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji Baraza la Wazazi Taifa, Mgore Miraji, ameendesha harambee na kufanikisha kupatikana usafiri wa bajaj ya mradi wa wenyeviti wa mitaa.

Wenyeviti wa mitaa manispaa ya Musoma walianzisha umoja huo ili kuweza kutatua changamoto zao mbalimbali zikiwemo za utekelezaji wa majukumu yao

Akizungumza na wenyeviti hao mara baada ya kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 8 kwaajili ya ununuzi wa usafiri huo,Mgore amesema wenyeviti wa mitaa wanafanya kazi kubwa hivyo wanapaswa kuangaliwa.

Amesema jukumu la kuwahudumia wananchi kwa shughuli za kila siku ni gumu huku ikizingatiwa huduma inaendana na vitendea kazi.

Mgore amesema wenyeviti wa mitaa ya manispaa ya Musoma hawana utaratibu wa posho za kazi kwaajili ya kutekeleza majukumu yao na kuwafanya kufanya kazi zao kwa ugumu.

Amesema mradi huo wa usafiri wa bajaj utawasaidia kuweza kupata mahitaji kama karatasi na vitendea kazi vingine wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Nawashukuru wenyeviti wa mitaa kunialika kwenye uzinduzi wa umoja wenu na kuniomba niendeshe harambee kwaajili ya kupata miradi ya umoja wenu.

Mmeomba mradi wa mashine ya kusaga nafaka pamoja na bajaj ya abiria lakini kwa leo tuanze na upatikanaji wa bajaj na baadae tupate mashine ya kusaga nafaka” amesema Mgore.

Baada ya makusanyo ya harambee hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Musoma club ,Mgore alikusanya kiasi cha shilingi milioni 6 na kuchangia milioni 2 ili bajaj hiyo iweze kupatikana.

Mwenyekiti wa umoja huo wa wenyeviti,Kizito Majumbi, amemshukuru kiongozi huyo kutoka baraza la wazazi taifa kwa kuona umuhimu wa wenyeviti wa mitaa na kuamua kuwashika mkono.

Amesema wenyeviti wa mitaa manispaa ya Musoma wanazo changamoto nyingi nakumuomba kuzifikisha ngazi ya taifa ikiwa ni pamoja na kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,na kwenye vikao vya jumuiya ya wazazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!