Na Shomari Binda-Musoma
MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Mgore Miraji amechangia thamani za ofisi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) tawi la Kiara B ili kukiimalisha chama.
Thamani hizo vikiwemo viti 6, meza,k aratasi na “file” vimekabidhiwa kwa niaba yake na diwani wa viti maalumu manispaa ya Musoma, Asha Muhamed kwa viongozi wa tawi hilo.
Asha amesema huo ni utekeleza wa kiongozi huyo baada ya kutoa ahadi ya kuchangia thamani za ofisi hiyo kama alivyoahidi hivi karibuni.
Amesema kiongozi mzuri ni yule anayeahidi na kutekeleza kama ambavyo amefanya mjumbe huyo wa kamati ya utekelezaji taifa wa jumuiya ya wazazi.
“Mheshimiwa Mgore yupo kwenye majukumu mengine na ameniagiza hapa Kiara kuja kukabidhi vifaa hivi kama ambavyo aliahidi” amesema Asha.
Mwenyekuti wa CCM wilaya ya Musoma Magiri Benedict, amesema kiongozi huyo anapaswa kupewa cheti cha shukrani kwa kukichangia chama.
Amesema chama bado kinahitaji michango ya wanachama wake hasa kuchangia kwenye matawi ili viongozi wake wafanye kazi za chama.
Magiri amesema wanachama wanaokichangia chama wasiusishwe na kutaka kugombea nafasi mbalimbali bali wapewe moyo wa kuendelea kuchanga.
Kwa upande wao viongozi wa CCM tawi hilo la Kiara B wamemshukuru,Mgore kwa kuwachangia thamani hizo za ofisi ili waweze kutimiza majukumu yao ya chama.