Home Kitaifa MGOMBEA WA CCM NJOFU COSTANTINE ASHINDA KWA KISHINDO UDIWANI KATA YA MSHIKAMANO

MGOMBEA WA CCM NJOFU COSTANTINE ASHINDA KWA KISHINDO UDIWANI KATA YA MSHIKAMANO

AWASHUKURU WANANCHI KWA KUMUAMINI

Na Shomari Binda-Musoma

MGOMBEA udiwani Kata ya Mshikamano manispaa ya Musoma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Njofu Constantine ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 885

Njofu amewashinda wagombea 9 wa vyama vya upinzani vilivyoshiriki kwenye uchaguzi huo mdogo uliofanyika kufuatia kifo cha diwani aliyekuwepo Charles Mwita.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi msaidizi wa uchaguzi Nanyika Chaki amemtangaza mgombea Njofu Constantine wa CCM kuwa mshindi kwa kupata kura 885

Mgombea wa Chama cha NCCR-Mageuzi Kafwemba Wang’ubha ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 445 kwenye uchaguzi huo

Wagombea wengine walioshiriki kwenye uchaguzi huo ni Christina Ndengo wa SAU aliyepata kura 8, Christopher Matofali wa CUF aliyepata kura 8, Rashid Ndaro wa UMD kura 4, Nicolaus Marichor wa NRA kura 3, Rutaga Sospeter wa AAFP kura 3, Omar Muhamed wa Demokrasia Makini kura 2, Malima Bulemo wa SP kura 2 na Davies Masiku wa UDP kura 1

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo mshindi wa uchaguzi huo Njofu Constantine wa CCM amewashukuru wananchi wa Kata ya Mshikamano kwa kumuamini na kumchagua.

Amesema imani walioionyesha kwake ni kubwa na kilichobaki ni kushirikiana nao kuleta maendeleo ya pamoja

Njofu amesema kama alivyokuwa akieleza kwenye kampeni uongozi wake utakuwa kwa wananchi wote wa Mshikamano bila kujali itikadi ya vyama vya kisiasa

Uchaguzi umekwisha hakuna tofauti zozote sasa ni kazi ya kushirikiana kwa pamoja kuweza kuwaletea wananchi maendeleo” amesema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!