Home Kimataifa MGINI KUJA NA MIPANGO YA UWEZESHAJI WAANDISHI BAADA YA USHINDI ( MRPC)

MGINI KUJA NA MIPANGO YA UWEZESHAJI WAANDISHI BAADA YA USHINDI ( MRPC)

Na Shomari Binda-Musoma

MWENYEKITI mpya wa klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mara ( MRPC) Mgini Jocob amesema moja ya mipango yake ni kuona Waandishi wa Habari mkoa wa Mara wananufaika kitaaluma na kiuchumi.

Kauli hiyo ameitoa hii leo juni 7 baada ya kushinda nafasi hiyo kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika ukumbi wa Fugo hotel mjini hapa

Amesema Waandishi wa Habari mkoa wa Mara wameendelea kumuamini na kumpa nafasi hiyo hivyo ni muhimu kurudisha fadhira.

Mgini amesema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na viongozi wengine wa MRPC atahakikisha maafunzo ya kitaaluma na fursa za kiuchumi wanazipata.

Amesema upendo unapaswa kuwa kwa kila Muandishi na kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuweza kufikia malengo anayo yakukusudia.

” Niwashukuru sana ndugu zangu kwa kuniamini na kunichagua kwenye nafasi hii nami naahidi tutashirikiana kuhakikisha klab yetu inakuwa ya mfano.

” Tutatafuta fursa za kitaaluma na kiuchumi ila tunapokuwa tunatekeleza majukumu yetu tufanye kwa ufanisi mkubwa”,amesema.

Kwenye uchaguzi huo mdogo wa MRPC ilikuwa ikijazwa nafasi ya Mwenyekiti kufuatia aliyekuwepo kusimamishwa na nafasi moja ya ujumbe ambaye slifariki dunia.

Mgini amemshinda Antony Mayunga kwa kupata kura 14 dhidi ya 10 za mpinzani wake huku Muhamed Nyabange akipata kura 12 kwenye nafasi ya ujumbe dhidi ya Ghati Msamba aliyepata kura 11

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!