Home Kitaifa MGAO WA MAJI WILAYA YA SERENGETI KUMALIZIKA HIVI KARIBUNI

MGAO WA MAJI WILAYA YA SERENGETI KUMALIZIKA HIVI KARIBUNI

Na Shomari Binda-Musoma

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (Muwasa) imesema mgao wa maji katikaa mji wa Mugumu wilayani Serengeti utamalizika hivi karibuni.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hiyo Mhandisi, Nicas Mugisha alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya tatizo la maji wilayani humo.

Amesema ni kweli kuna changamoto ya maji kwa baadhi ya maeneo kupata maji kwa mgao wilayani Serengeti lakini tatizo hilo linafanyiwa kazi.

Nicas amesema tatizo hilo linatokana na kutumika kwa pampu moja kupeleka maji kwenye tenki la DDH na kwa sasa inasubiliwa pampu ya pili.

Amesema pampu ya pili imeshaagizwa na itafika baada ya wiki mbili na itakapofungwa tatizo hilo la mgao litamalizika na wananchi watapata maji kwa uhakika.

“Ni kweli kuna changamoto ya mgao wa maji kwenye baadhi ya maeneo wilayani Serengeti na tatizo hili litakwenda kumalizika hivi karibuni”

“Tunaomba radhi kwa tatizo hili lakini linashughulikiwa na wananchi watapata maji kama ambavyo imekusudiwa na serikali kuwafikishia wananchi huduma”, amesema Nicas.

Mkurugenzi huyo amesema changamoto hiyo itakwisha baada ya pampu hiyo iliyoharobika itakapofika na kufungwa.

Amesema tatizo la pili pamoja na mgao huo ni kutokuwepo kwa ratiba inayoeleweka ya mgao kwenye mitaa husika ambapo jambo hilo linafanyiwa kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!