Mei 29, 2024, imeamuliwa Kesi ya Jinai Na.CC. 12307/2024 mbele ya Mh. Sydney Nindi .
Katika Shauri hilo lililoendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Amos Mwalwanda, Washtakiwa Pius Emmanuel Lyambise na Nestori Fransisko Gabulieli (Mgambo wa Kijiji cha Majalila), walishtakiwa kwa kosa la kuomba hongo ya sh. 200,000/= kinyume na Kifungu cha 15 (1) (a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya 2022.
Ilielezwa, mnamo Aprili 25, 2024, Washtakiwa waliomba hongo hiyo kutoka kwa David Elias Shem na Alphans Japhet Bwangaro ili wawaachie baada ya kuwakamata wakisafirisha mbao kutoka Tanganyika kwenda Mpanda bila kibali.
Mahakama imewahukumu kulipa faini ya Shilingi 500,000/= kila mmoja au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
Washtakiwa wamelipa faini ya shilingi 500,000/= kwa kila mshtakiwa.