Na Boniface Gideon, TANGA
MGAHAWA wa ARBAB TANGA SEA FOOD & MORE ambao unakuwa mgahawa wa kwanza unaotoa huduma za vyakula vya asili vinavyotokana na Rasilimali za Bahari ya Hindi umezinduliwa rasmi Jijini Tanga na unatarajiwa kutoa huduma za vyakula vya asili kwa Watalii wa ndani na nje ya Nchi.
Kwamujibu wa waandaji wa mgahawa huo wanaeleza kuwa Utakuwa Mgahawa maalumu kwa asilimia 90 kutoa huduma za vyakula vya viumbe Bahari na umezingatia utamaduni wa Maisha ya Jamii ya Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba Jana Wakati wa uzinduzi wa mgahawa huo alipongeza waandaji wa mgahawa huo kwakubuni na kuona fursa za Kiuchumi zinazotokana na Rasilimali Bahari,
“Nikupongeze ndugu yangu ARBAB kwakuja na wazo hili na ukathubutu kufanya kitu hiki kikubwa , Nikuahidi tu kuwa Serikali itakulinda kwakuhakikisha unapata wateja Wengi zaidi na pia hakuna Biashara itakayofungwa iwe ndogo au kubwa na tutahakikisha tunawalinda Wafabiashara wote ili waongez