Home Kitaifa Mfumo wa kukusanya Mapato kufika sehemu zote nchini

Mfumo wa kukusanya Mapato kufika sehemu zote nchini

Na Neema Kandoro Mwanza

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inakusudia kufikisha mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki sehemu zote hapa nchini ili kuondoa mianya ya upotevu wa fedha na kukuza uchumi.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni Jijini Mwanza katika mafunzo kwa watendaji wa halmashauri 57 kutoka katika mikoa saba iliyolenga kuwajengea maarifa ya usimamizi wa fedha na ukusanyaji mapato kwa wahasibu na watunza fedha.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa fedha TAMISEMI Ummy Wayayu alisema kuwa lengo hilo litawezesha serikali kukusanya fedha nyingi toka katika maeneo mengi ambayo yalikuwa na changamoto ya kufikiwa kwa ufanisi zaidi.

Alisema kuanzia mwaka ujao mfumo huo utawezesha fedha kuanzia ngazi za mitaa, vijiji na mitaa zinazokusanywa kuwekwa benki kwa wakati hivyo kuepesha upotevu wa mapato na kuwezesha TAMISEMI kufahamu makusanyo hayo kila siku.

Wayayu aliongeza kusema maboresho hayo yatawezesha wafanyabiashara kuomba leseni zao kwa njia ya kielektroniki kwa haraka zaidi na kuondoa changamoto iliyokuwa ikijitokeza ya kuchelewa kupata huduma hiyo.

Mfumo wa Uhasibu na Utoaji wa Taarifa za fedha kwa Ngazi ya vituo vya utoaji huduma (FFARS) ulioboreshwa utafikishwa katika ngazi zote hapa nchini mwakani ili kuboresha mfumo wa ukusanyaji mapato” alisema Wayayu.

Afisa Usimamizi wa Fedha TAMISEMI Eusa Rwamiago aliwaomba wakurugenzi kuhakikisha kuwa wanawezesha upatikanaji wa haraka kwa leseni za wafanyabiashara ili kuwezesha ufanisi mkubwa wa kuongeza makusanyo ya mapato nchini.

Rwamiago alisema lengo la TAMISEMI ni kutaka wahasibu na watunza fedha kuhakisha kuwa wanatimiza malengo yao kwa wakati kabla ya mwaka fedha ili kuepusha upotevu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!