Home Michezo MEYA GUMBO AFUNGUA MASHINDANO YA MATHAYO CUP 2023 KWA KUWAPA UJUMBE WACHEZAJI

MEYA GUMBO AFUNGUA MASHINDANO YA MATHAYO CUP 2023 KWA KUWAPA UJUMBE WACHEZAJI

Na Shomari Binda-Musoma

MASHINDANO ya kombe la Mathayo Cup 2023 yamezinduliwa rasmi na Meya wa manispaa ya Musoma, Patrick Gumbo huku vijana wakitakiwa kuyatumia kuinua vipaji.

Jumla ya Kata 16 za jimbo la Musoma mjini zinashiriki mashindano hayo ambapo kila timu imekabidhiwa seti ya jezi na mipira miwili.

Akifungua mashindano hayo kwenye uwanja wa Posta, Meya Gumbo amesema licha ya timu kupewa vifaa lakini zawadi zimeboreshwa tofauti na msimu uliopita.

Amesema bingwa wa msimu huu ataondoka na zawadi ya ng’ombe mkubwa na mshindi wa pili ataondoka na zawadi ya shilingi laki 5 na mbuzi mmoja huku mshindi wa pili akiondoka na shilingi laki 3 na mbuzi mmoja.

Aidha Meya Gumbo amesema licha ya zawadi hizo kwa timu kutakuwa na zawadi kwa timu yenye nidhamu,mchezaji bora,mfungaji bora na mchezaji bora wa mashindano.

“Tunaendelea kumshukuru mheshimiwa mbunge kwa namna anavyowathamini vijana kwenye masuala mbalimbali yakiwemo ya kimichezo”

“Mashindano ya mwaka huu yameboreshwa zaidi na zawadi ni kubwa hivyo kila timu iwe tayari kushiriki kwa nidhamu ya hali ya huu” amesema Meya Gumbo.

Baadhi ya mashabiki waliohudhuria ufunguzi huo wamemshukuru mbunge Mathayo kwa kuwaletea burudani na kuinua vipaji vya vijana.

Katika mchezo wa ufunguzi uliokutanisha timu za mashabiki wa Simba na Yanga umeshuhudia timu ya mashabiki wa Yanga wakichomoza na ushindi wa bao 1-0 na kuondoka na zawadi ya mbuzi 2 na Simba mbuzi 1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!