Home Kitaifa Meli ya kubeba Mizigo Tani 1200 MV umoja yakamilika na kuzinduliwa Mwanza...

Meli ya kubeba Mizigo Tani 1200 MV umoja yakamilika na kuzinduliwa Mwanza 17/11/2023

Neema Kandoro Mwanza

UKARABATI wa meli ya kubeba mizigo tani 1200 MV Umoja umekamilika na kuzinduliwa kwa ajili ya kuanza kutoa huduma zake toka Jijini Mwanza kwenda bandari za mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki.

Meli hiyo ambayo kwa sasa itaitwa “MV New Umoja Kazi Iendelee” imekarabatiwa kwa sh bilioni 21 na itakuwa ikisafiri kwa saa 13 kufika nchini Uganda badala ya saa 24.

Mkurugenzi wa Shirika la Huduma za Meli Hamis Erick alisema kuwa meli hiyo itatoa huduma kwenye ushoroba wa Kati na tayari imeshaanza kufanya majaribio ya kupeleka mizigo kwenye bandari za Port Bell, Jinja na Kisumu.

Sambamba na uzinduzi wa meli hiyo vilevile kulifanyika utiaji saini mikataba ya ukarabati wa MT Nyangumi kwa bilioni 7.2 na MT Ukerewe kwa bilioni 6.3 na MV Liemba itakayofanya kazi kwenye Ziwa Tanganyika ukiwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 200 za mizigo.

Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile alisema kuwa haya ni mafanikio makubwa kwani usafiri majini una mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi hapa nchini.

Alisema kukamilika kwa ukarabati wa meli hiyo utakuwa ni kiungo kikubwa katika reli ya kati ambayo unafanyika Ujenzi wa SGR hivyo itaunganisha miundombinu ya usafiri kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi alipongeza hatua hiyo kwa kusema kuwa mradi huo ni kichocheo cha uchumi wa eneo hilo na hivyo kuomba jitihada hizo za kuleta mapinduzi kwa usafiri wa majini ziendelezwe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!