Home Kitaifa MDAU WA MAENDELEO ENOCK KOOLA AJIUNGA NA WANANCHI KUCHANGIA UJENZI WA MFEREJI...

MDAU WA MAENDELEO ENOCK KOOLA AJIUNGA NA WANANCHI KUCHANGIA UJENZI WA MFEREJI WA USHIRIKA MAKUYUNI.

Ashrack Miraji () Kilimanjaro

Wanachama wa Ushirika Wametoa shukran za dhati Kwa Mdau huyo Kushiriki zoezi la Ujenzi wa Mfereji ambao unaohudumia zaidi ya kaya 500 kata ya Makuyuni wilaya ya Moshi vijijini Mkoani Kilimanjaro Mfereji huo wa Maji walikuwa wanautumia Kwa shughuli Mbalimbali za kijamii kama kilimo Cha mboga mboga na kunyweshwea mifugo

Akizungumza Kwa njia ya simu na kituo hiki koola alisema wanachama walijikuta katika wakati mgumu baada ya birika linalovusha maji kuharibika vibaya na kushindwa kuvusha maji kwenda kwenye mfereji huo na kuleta changamoto hiyo ambayo imejitokeza kwa Mara ya pili sasa.

viongozi hao waliitaarifu bodi ya tume ya umwagiliaji walifika na kuangalia adhari hizo na kutoa ushauri ukarabati mkubwa ufanyike kwa dharura ili wananchi waendelee kupata huduma ya Maji ya kumwagilia na kunyweshea mifugo Yao.. alisema Ndugu Koola

“Ni furaha kwangu kuona changamoto za wananchi wenzangu zinatatuliwa kwa wakati ndio maana pale ninaposhirikishwa na viongozi mbali mbali iwe wa dini,wa jamii au wa chama Basi lazima nishirikiane nao kutatua changamoto husika.”Koola

Nafanya haya Kwa lengo la kushirikiana serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na kinara wetu hodari Mhe Rais wa jamuhur ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mfano Bora wa kuigwa hasa Katika Taifa letu tumeona na kushuhudia kiasi gani anapambana Katika kuleta Maendeleo kwenye Taifa letu hivyo ni jitihada zetu kumuunga Mkono Mhe Rais.

Sambamba na hayo yote Baadhi ya viongozi wa mfereji huo wakiongozwa na Jafar mfinanga waliitisha mkutano wa watumiaji wa Mfereji huo na Wadau Mbalimbali lengo kuweza kusaidiwa kukarabati miundombinu ya Mfereji huo kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa haraka ,

” tuliwasiliana na Mh naibu Waziri Ummyu ambaye ni mzaliwa wa Makuyuni na aliahidi kutuchangia Tsh laki mbili, pamoja na mh Diwani akatuchangia sh laki moja na nusu,Mama Santorin akatuchangia sh laki mbili,*Pia tulimpigia mdau wa maendeleo ndugu Enock Koola na kwa haraka alikubali kushirikiana na wananchi wa kata ya Makuyuni kwa kuchangia sh laki tano na kuahidi atashirikiana nasi zaidi endapo tukikwama Kwa mara nyingine”
“Alisema mfinanga “

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!