Home Michezo MCHEZAJI WA ZAMANI WA KLABU YA SIMBA, JOHN BOCCO KUICHEZEA JKT

MCHEZAJI WA ZAMANI WA KLABU YA SIMBA, JOHN BOCCO KUICHEZEA JKT

Na Magrethy Katengu– Dar es Salaam

JKT Tanzania wamesajili wachezaji akiwemo aliyekuwa mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba John Raphael Bocco kwani alikuwa huru na wanaimani kupitia kiwango chake timu itafika mahali pazuri kwa kupata kombe au kuwa katika nafasi kuanzia ya nne hadi ya kwanza.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo julai 10, 2024 Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa hiyo Msemaji wa timu ya JKT Tanzania Masau Bwire amesema timu hiyo imekuwa ya kizalendo inajali wazawa na haina mchezaji hata mmoja kutoka nje ya nchi wanaimani na vipaji vya watanzania wenyewe.

“Bocco mliemtazama katika msimu uliopita mliona kazi yake niseme kwamba huku amezaliwa upya, kwani baada ya usajili tu yeye alikuwa wa kwanza kufika kambini tulianza naye na ameonesha nidhamu ya hali ya juu” amesema msemaji wa JKT

Pia wamemsajili mchezaji kutoka Uhamiaji Zanzibar, Charse Ilamfya kutoka mtibwa, Kipata KMC Denisi Richard, Karimu Mfaume Fikiri kutoka biashara, Twalupo Elisha Jafeti, Hamisi Salum Hamisi-,Kombo Hatibu anamalizia mafunzo ya kijeshi, TMA ya Arusha Wilson Nangu.

“Tunao wachezaji wengine takribani wawili bado tunaendelea kukamilisha mchakato wa usajili wao kutoka katika timu zao, sisi ni timu ambayo tunapenda kukamilisha taratibu za kuhamisha wachezaji hatupendi mitifuano na mvurugano kwetu maridhiano ndio jambo la msingi” amesema Bwire

Bwire ameongeza kuwa JKT Tanzania wanatengeneza uwanja wenye viwango vya kimataifa ambapo utaambatana na VVIP ambao mtazamaji wa mpira akikaa kwenye jukwaa ataburudika na vitu vingi upande mmoja utakuwa ataburudika na zoo, na upande mwingine bahari utakuwa ni uwanja wa aina yake.

Hata hivyo amebainisha kuwa ifikapo mwezi wa nane uwanja utakuwa umekamilika ambapo wanategemea mashabiki elfu nane 8 hadi elfu kumi 10 watakaa kwa nafasi bila kubughudhiwa wakitazama soka.

Katika hatua nyingine JKT Tanzania imetangaza rasmi kubadili mfumo wa uongozi katika klabu hiyo pamoja na klabu ya JKT Queens na ambapo zitakuwa na uongozi wa pamoja tofauti na hapo awali ambapo kila klabu ilijitegemea.

Msemaji wa timu ya JKT Tanzania Masau Bwire Amesema wamefanya mabadiliko mbalimbali ikiwemo katika nafasi za uongozi ikiwemo :- Mlezi wa timu zote mbili ni Hassani Rashidi Mabeyo, Mwenyekiti wa Bodi ni Kanali Jophrey Roidi Mvula, Wajumbe wa bodi ni Luteni Kanali Mkuu, Luten Kanali Salumu Mangapi, Meja Salumu Chamsam, Mtendaji mkuu wa JKT Tanzania ni Jemedari Saidy Kazumali.

Masau ameongeza kuwa utaratibu umebadilika katika uendeshaji wa timu hizo katika nafasi hizo ambapo nafasi nyingine zimeongezwa na nyingine zimepunguzwa ambapo kumeongezeka nafasi ya waratibu wa timu ambapo watakuwa na wajibu wa kuripoti kwa Mkurugenzi mkuu.

Mratibu upande wa JKT Tanzania ni Stan Joseph Chahe, na kwa upande wa JKT Queens ni Meja Esta Rioba,

Pia kuna idara mbalimbali ikiwemo Mkurugenzi wa ufundi ambapo itasimamiwa na Mwalimu Hamadi ally, kurugenzi ya mashindano, fedha Meja innocent Ndunguru,sheria Captein Immaculate Ediga Mapunda,masoko Sekeratusi Mengela Lubinga na idara ya habari na mawasiliano Masau Bwire

Aidha amebainisha kuwa watakuwa na siku ya wazalendo ambapo itafanyika kwa upekee wake hivyo wapenzi wa burudani wasikose

“Kuna timu wanajiita wananchi kuna wengine wanajiita wenyenchi mimi sijui wametoa wapi haya majina lakini sisi JKT Tanzania ni wazalendo, sisi ndio klabu pekee yenye viongozi na wachezaji kutoka ndani ya nchi hakuna hata mmoja kutoka nje, sasa sisi wazalendo tutawaoneshe”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!