KUELEKEA pambano la Kitaifa kati ya Twaha Kiduku na Bondia kutoka Misri Abdo Khaled wanamichezo hususani mchezo wa Masumbwi wametakiwa kuvunja matabaka na kuungana Kwa pamoja na kumtakia heri bondia Twaha Kiduku kufanya vizuri septemba 24 katika viwanja vya Nangwanda sijaona Mkoani Mtwara kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.
Akizungumza Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amesema makando kando Hayana Msingi pale Taifa linapomteua mtu akatuwakilishe kitaifa katika Michezo badala yake nguvu na hamasa zitumike kumpa moyo wa kufanya vizuri mchezaji huyo.
Hata hivyo ameeleza kuwa Wizara yake itampa ushirikiano wa kutosha na inamuunga Mkono Bondia huyo ili kuleta chachu ya ushindi wake ambao Taifa litajuvunia kutokana na ubingwa wake katika mchezo wa Masumbwi nchini.
Aidha amemtaja Kiduku ambae ana wania mkanda wa UBO ni Miongoni mwa Mabondia wanaofanya vizuri ambao kimsingi anatambua nafasi yake katika kuweka Ramani ya Mchezo wa Masumbwi Kitaifa na Kimataifa.
“Anapokuwa ulingoni anafanya vizuri na unamuona ana kiu yakuhitaji ushindi hivyo wizara kwa pamoja tunamuunga mkono na kumtakia ushindi dhidi ya mpinzani wake kutoka Misri kwani ushindi wake ni wataifa kwa ujumla sio wake peke yake.”
Pia ametoa wito kwa viongozi wa halmashauri,wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuwaeka pamoja na kuwapa hamasa wananchi wao kushiriki katika Michezo mbalimbali ili kuimarisha miili yao.
MCHENGERWA AUNGANA NA TWAHA KIDUKU PAMBANO LA UBABE UBABE 2

“Tunaibeba kauli mbiu ya pambano hili “Ubabe ubabe tu” iende katika kila wilaya,mikoa na kila mitaa ikaamshe vipaji vingine katika Michezo na pia viongozi kwa ujumla wahakikishe wanaleta hamasa kwa wananchi wao kuhakikisha Michezo inapewa nafasi kubwa kwenye jamii.”