Home Kitaifa MBUNGE WA LUSHOTO AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA AMBAO...

MBUNGE WA LUSHOTO AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA AMBAO UNATARAJIA KUFANYIKA NOVEMBER 27

Na Ashrack Miraji, (Fullshangwe Media)

Mbuge wa Jimbo la Lushoto Mhe Alhaj Shabani Omary Shekirindi amewasihi wananchi wa Jimbo hilo kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utafanyika mnamo tarehe 27 November mwaka huu.

Mheshimiwa Shekirindi ameyasema hayo Wakati akishiriki hadhara ya Maulid iliyoandaliwa na wanawake wa kata ya Mlola Kitongoji cha hondelo wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

“Nitumie fursa hii pia kuwapongeza akina Mama wa kitongoji hiki kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya lakini pia niwaombe akina mama kushiriki Katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kwa kuchagua Viongozi Bora wenye maslahi mapana ya Taifa letu na kuleta Maendeleo tuache Viongozi wanao toa rushwa Kwa maslahi Yao binafsi na pia kumpongeza Mhe Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kazi kubwa anayoifanya Leo tumeona anajenga Barabara kubwa na ya kisasa hii ni Kwa ajili yenu kina Mama mpate Huduma za kijamii na wafanyabiashara kufungua fursa za kiuchumi Katika Kata hii”
“Alisema Mbunge huyo”.

“Mimi kama Mbuge wenu naendelea kupambana Kwa Hali na Mali baada ya kukamilika ujenzi wa Barabara ambayo ilikuwa kero ya muda mrefu Sasa inakwenda kukamilika na kuunganisha Kata na vijiji Sasa napambana kuleta umeme Kwa Wakazi wa vijiji hivi ambavyo vipo kwenye Jimbo langu”

Sambamba na hayo ametoa onyo Kali Kwa Baadhi ya Viongozi wanaosema Barabara hiyo wanajenga Kwa nguvu zao Kwa lengo la kutaka kuwarubuni wananchi hivyo kuwataka wananchi hao kuwa makini na upotoshwajwi unaofanywa na baadhi ya viongozi hao juu ya ujenzi wa barabara hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!