Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini,Profesa Sospeter Muhongo,anatarajiwa kuongoza harambee ya ujenzi sekonari jimboni humo.
Harambee ya kwanza itakayoongozwa na mbunge huyo itafanyika kisiwani Rukuba kwa ujenzi wa shule ya sekondari Rukuba.
Harambee ya ujenzi wa sekondari hii utafanyika septemba 27 kisiwani hapo huku tayari wanakijiji wa kisiwa hicho wakiwa tayari wameanza kujitolea nguvu kazi kwa kusomba mawe.
Licha ya kuchangia mawe imetolewa akaunti ya kucjqngia kwenye benki ya NMB yenye akaunti ya serikali ya Kijiji kwa namba 30302300701.
Harambee ya 2 ataiongoza septemba 29 katika Kijiji cha Kurwaki huku wananchi pia wakiwa wameanza kuchangia nguvu Nazi kwa kusomba mawe.
Kijiji cha Kurwaki kinajianda kujenga sekondari ya kumbukumbu ya Profesa Massamba aliyefariki hivi karibuni.
Tayari akaunti ya serikali ya Kijiji kwenye benki ya NMB yenye namba 30302301539 imefunguliwa kwaajili ya kuchangia.
Mbunge huyo wa jimbo LA Musoma vijijini amesema elimu in kipaumbele na ujenzi wa shule lazima.uendelee.
Muhongo amewakaribisha wadau mbalimbali na wananchi wa vijiji hivyo kujitokeza kuchangia ujenzi wa shule hizo.