-MBUNGE SAGINI ASEMA HATENDEWI HAKI
Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo ametaka mchango wake na ile ya wananchi kwa kuchangia miradi ya maendeleo itambulike.
Akichangia kwenye kikao cha ushauri cha mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa uwekezaji wa mkoa amesema halmashauri imekuwa haitambui kinachofanyika kwenye miradi husika.
Amesema alikuwa akikaa kimya lakini imemlazimu kuongea kwa kuwa yeye pamoja na wananchi wamekuwa wakichangia lakini michango imekuwa haitambuliki.
Muhongo amesema kwenye elimu amekuwa akiendesha harambee za kuchangia kwa kushirikiana na wananchi lakini halmashauri licha ya kutokuchangia inashindwa kutambua hata michango inayotolewa.
Mbunge huyo amesema licha ya changamoto hizo hajaweza kukatishwa tamaa kuendelea kuchangia miradi ya maendeleo kwa kushirikiana na wananchi.
Amesema harambee nyingi amezifanya kwa kushirikiana na wananchi halmashauri hata cheti cha shukrani hakijawahi kutolewa kwa out am bus michango hiyo.
“Mwenyekiti mimi na wananchi tumekuwa tukichangia miradi ya maendeleo ikiwemo ya elimu,maji na afya lakini michango yote haitambuliwi.
“Sio kwamba wananchi hawachangii lakini yapo mambo ambayo yanakatisha tamaa ikiwa hata kutambua mchango hautambuliwi.
Mbunge wa jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini amesema kutokutambua mchango wa mbunge Muhongo ni kutomtendea haki.
Amesema kwa upande wake halmashauri ya Butiama imekuwa ikitambua mchango anaotoa yeye pamoja na wananchi na imekuwa ikitia moyo.
Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda amesema mbunge Muhongo amekuwa akifanya jitihada kubwa za kuchangia shughuli za maendeleo na mchango wake lazima utambulike.
Amesema taarifa za mbunge huyo amekuwa akiziona mbunge huuo anapozituma zikiwemo za harambee na kuto kutambua mchango wake sio jambo jema.