Home Kitaifa MBUNGE MSTAAFU JIMBO LA NGARA AYATAJA MAFANIKIO YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA...

MBUNGE MSTAAFU JIMBO LA NGARA AYATAJA MAFANIKIO YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Na Theophilida Felician Kagera.

Pius B. Ngeze ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Ngara Mkoani Kagera ameyaeleza mafanikio kadha wa kadha yaliopatikana tangu kuungana kwa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar tangu nchi hizo zilipoungana mnamo Tarehe 26/4/1964.

Ngeze ambaye amewahi kuzitumikia nyadhifa mbalimbali ikiwemo ya kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa Kagera kwa kipindi cha miaka 25 kuanzia mwaka (1977)hadi (1992) ameyasema hayo wakati akihojiwa na Blog hii ofisini kwake Mjini Bukoba.

Ameeleza kwamba leo nchi ya Tanzania inaazimisha shehere za Muungano kwa muda wa kipindi cha miaka (59) kukiwa kumejaa mafanikio tele yanayoonekana kwa nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar.

Baadhi ya mafanikio ameyataja kuwa ni kudumisha Muungano kwa muda mrefu jambo ambalo limewashinda wengine “sisi tumeliweza kuna nchi ziliungana na baada ya muda mfupi zika vunja muungano kwetu hii ni hatua kubwa sana si jambo dogo hata kidogo tangu mwaka (1964) walivyotuunganisha waasisi wetu tumeendelea kuwa wa moja hiyo ikiwa sambamba na kuwepo kwa amani na utulivu wa hali ya juu”amesema Pius Ngeze.

Mafanikio mengine amesema kuwa serikali imefanikiwa kufanya mengi ya maendeleo ya wananchi kwani kwa sasa Tanzania kwa Afrika Mashariki ndo nchi inayo paa kwa kasi katika ukuaji kiuchumi kupitia nyanja tofauti tofauti hususani elimu, afya, kilimo, viwanda, uwekezaji pamoja na kuikuza lugha ya kiswahili ndani ya nchi na mataifa mbalimbali Duniani.

Jambo jingine amelitaja kuwa nchi zimeendelea kuongozwa na chama cha mapinduzi (CCM) chama ambacho kimekuwa na nguvu imara katika kuisimamia Serikali hatimaye viongozi wakaendelea kuongoza kwa amani mshikamano na umoja kwa watanzania wote.

Amesema kuwa licha ya mafanikio hayo ya Muungano wakati mwingine hujitokeza kelo za hapa na pale kutoka kwa wananchi wakilalamikia baadhi ya mambo na hutatuliwa na kuyaweka sawa.

Amemshukuru na kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa namna anavyoendelea kuchapa kazi ya kuiongoza nchi kwakuzingatia misingi ya sheria na katiba ya nchi kwakufanya hivyo Tanzania ataivusha na kuifikisha mbali kimaendeleo.

“Mama anachokifanya sasa ni chakushangaza macho yawaliowengi awali baadhi ya watu hawakuamini kama nchi itaimalika namna hii walibeza sasa ona wameduaa”! Mzee Ngeze akiendelea kueleza.

Amewaomba viongozi wote Tanzania kuendelea kushikamana na kulijenga Taifa kwa umoja na mshikamano kama yalivyokuwa matakwa ya waasisi wa Muungano Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Rais wa kwanza wa Tanganyika pamoja naye hayati Sheikh Abeid Amani Karume Rais wa kwanza Zanzibar

Amehitimisha akitoa wito kwa wananchi hasa hasa vijana wasomi na wasio wasomi kujimudu na kufanya kazi mbalimbali za kujiingizia kipato badala ya kukaa tuu wakingojea ajira huku akiiomba Serikali kuwajengea uwezo wa kujiajili vijana wanaohitimu mafunzo ya ujuzi katika vyuo vya kati na vikuu sambamba na masomo ya shule za Msingi na Sekondari.

Nao baadhi ya wananchi katika mitaa tofauti tofauti wakiendelea na kusherehekea sherehe hizo wameeleza kuwa wanawashukuru viongozi wote kwajinsi wanavyoendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi zote mbili kwani ni jambo ambalo wamelishuhia muda mrefu tangu kuungana kwa nchi hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!