Home Kitaifa MBUNGE MONNI AKABIDHI MADAWATI 200 SHULE ZA MSINGI CHEMBA

MBUNGE MONNI AKABIDHI MADAWATI 200 SHULE ZA MSINGI CHEMBA

Katika kukabiliana na Changamoto ya upungufu wa madawati katika halmashauri ya wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma Mbunge wa Jimbo la Chemba Mohamed Monni amekabidhi madawati 200 kwa shule sita za msingi Miongoni mwa shule hizo ni pamoja na mapango, Chinika, Kelema kuu, Parang, Rofati na Chukuruma

Mbunge huyo amekabidhi Madawati hayo leo Alhamisi Agosti 8, 2024 wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.

Akikabidhi madawati hayo yenye thamani ya shilingi milioni 20 Mbunge Monni amesema madawati hayo yatasaidia kupunguza uhaba huo wakati serikali ikifanya jitihada za kumaliza changamoto hiyo.

Amesema madawati hayo yatakuwa chachu kuongeza ufaulu kwa wananfunzi huku akiwataka wazazi, walezi kushirikiana na walimu katika kuwahamasisha wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuweza kujikwamuwa kiuchumi na kuondokana na wimbi la umaskini katika jamii ya watu wa Chemba

“Leo nimekabidhi madawati 200 kwa ajili ya shule sita za msingi katika halmashauri ya wilaya ya Chemba pamoja na jitihada za serikali kupambana na kuboresha miundombinu ya elimu niwaase vijana wangu msome kwa bidii, elimu ni msingi wa maisha lakini pia ndiyo chanzo kikuu cha maarifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!