Mbunge wa Jimbo la Chemba (CCM) Mohamed Monni amekabidhi mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya umaliziaji Ofisi na uanzishwaji wa ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Handa Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.
Pia Mbunge huyo amekabidhi Mashuka Seti kumi kwa ajili ya Zahanati ya kijiji cha Wairo na Milioni mbili umaliziaji ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya msingi Wairo iliyopo kata ya Lalta kijiji cha Wairo.
Akikabishi Mifuko hiyo ya Saruji leo Jumapili Agosti 11,2024 Mbunge Monni amesema zoezi hilo ni kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu ya elimu nchini.
“Namshukuru mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia kwa kuendelea kuleta fedha nyingi za miradi katika Kata hii ya Handa miongoni mwa fedha alizozitoa Rais Samia kukamilisha miradi ya maendeleo ni pamoja na Sh. Milioni Mia tano themanini na nne 584,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Msongi,”
“Na Milioni Mia tatu kumi na saba 317,000,000 Kwa ajili umaliziaji wa Shule ya Sekondari lakini pia Milioni hamsini na tatu 53,000,000/ kwa ajili madarasa na matundu ya vyoo shule ya Msingi Handa A,”
Amesema kazi Serikali ya Rais Samia nikumalizia miradi ambayo tayari yalishaanzishwa na wananchi hivyo niwaase wananchi wenzangu tufanye kazi kwa bidii Nakutunza miundombinu kwani imekuwa ikigharimu fedha nyingi za serikali