Home Kitaifa MBUNGE MATHAYO, MEYA GUMBO WAHAIDI KUZITAFUTIA UFUMBUZI KERO ZA WANANCHI

MBUNGE MATHAYO, MEYA GUMBO WAHAIDI KUZITAFUTIA UFUMBUZI KERO ZA WANANCHI

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo na Meya wa manispaa ya Musoma Patrick Gumbo wameahidi kuzitafutia ufumbuzi kero mbalimbali za wananchi.

Wakijibu kero mbalimbali za wananchi walizozitoa leo agosti 14 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Makoko wamesema kero za wananchi zinapaswa kutatuliwa na viongozi.

Katika mkutano huo wananchi wametoa kero mbalimbali ikiwemo migogoro ya viwanja na mikopo ya asilimia 10 itolewayo na halmashauri ya manispaa.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Amina Said amesema kero yake ni kiwanja chake kuingiliwa na kukosa njia ya kupitia

Akijibu kero hiyo pamoja nyingie Meya wa manispaa ya Musoma Patrick Gumbo amesema hakuna kero ambayo haita shughulikiwa kwa kuwa ndio kazi ya viongozi.

Gumbo ambaye pia ni diwani wa Kata ya Makoko amesema kero nyingi zimetatuliwa na miradi mingi ya maendeleo imepelekwa kwenye Kata ya Makoko.

Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema wananchi wasisubili mikutano ya hadhara kutoa kero kwa kuwa ofisi yake ipo wazi na wananchi wanasikilizwa na kutatuliwa kero zao.

Akizungumza maendeleo ya jimbo la Musoma mjini Mathayo amesema serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeotoa fedha nyingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amesema kwenye sekta ya maji jimbo la Musoma mjini ni jimbo pekee lenye mtandao wa maji kwa asiimia 98 na kwenye elimu,afya na miundombinu hali ni nzuri.

Mathayo amesema kabla ya kwenda bungeni ni utaratibu wake kuwasikiliza wananchi na amefanya hivyo kutembelea maeneo mbalimbali na anakwenda kuyafanyia kazi aliyoyapokea

Mkutano huo umehudhuriwa pia na mkuu wa wilaya ya Musoma Dk.Khafan Haule ambaye pia alipokea kero za wananchi pamoja na viongozi wengine wakiwemo madiwani wa manispaa ya Musoma

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!