Home Kitaifa MBUNGE MATHAYO KUBEBA DHAMANA YA MKOPO WA PIKIPIKI 160 KWA BODABODA JIMBO...

MBUNGE MATHAYO KUBEBA DHAMANA YA MKOPO WA PIKIPIKI 160 KWA BODABODA JIMBO LA MUSOMA MJINI KUTOKA BENKI YA AZANIA

-KUANZA NA MILIONI 24 AWAMU YA KWANZA

Na Shomari Binda-Musoma

KATIKA kuendelea kuwawezesha vijana kiuchumi mbunge wa jimbo la Musoma mjini amekuja na mpango wa kuwawezesha waendesha pikipiki”bodaboda” kupata mikopo.

Mikopo hiyo ya pikipiki jumla ya 160 zitakazo tolewa na benki ya Azania ni kutokana na mazungumzo ambayo yamefanywa baina ya mbunge na benki hiyo.

Akizungumza na bodaboda hao kwa niaba ya mbunge huyo kwenye ofisi za umoja wa bodaboda manispaa ya Musoma,mstahiki Meya Patrick Gumbo amesema mbunge ameiona fursa na kuamua kuileta kwa vijana.

Amesema mbunge akiwa kwenye maandalizi ya vikao vya bunge amekutana na uongozi wa benki ya Azania na kuzungumza nao utaratibu mzima wa kupata mikopo hiyo.

Gumbo amesema moja ya sharti la kupata mikopo hiyo ni kuunda vikundi vya watu 10 na kukamilisha vigezo vichache na kupokea mkopo wa pikipiki 5.

Amesema kila kikundi kinapaswa walau kuchangia kiasi cha shilingi laki 3 na mbunge kugharamikia laki 9 za awali ili pikipiki ziweze kuwafikia.

“Mbunge anatupenda ameiona fursa kutoka benki ya Azania na kutuletea na amenituma hapa kuja kuwapa utaratibu mzima”

“Tutakapo wekana sawa kuhusu utaratibu mzima tutawaita maafisa wa benki ya Azania na zoezi hili inatakiwa miezi 3 ya kwanza zitoke pikipiki 80 na miezi 3 mingine zitoke pikipiki 80” amesema Gumbo.

Amesema kwa kuwa moja ya sharti pia ni kuwa na leseni pamoja mbunge Vedastus Mathayo yupo tayari kuzungumza na mkuu wa usalama.barabarani pamoja na Veta ili agharamikie mafunzo na kupata leseni.

Akizungumza na vijana hao wa bodaboda kwa njia ya simu ya moja kwa moja kupitia mstahiki Meya mbunge Mathayo amesema wanapaswa kuchangamka kwa upande wao na watakao kuwa tayari watapata pikipiki hizo kwa wakati

Mwenyekiti wa umoja wa bodaboda manispaa ya Musoma Stephano Silas amemshukuru mbunge huyo kwa kuamua kuwapigania ili kuinua uchumi wa vijana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!