Home Michezo MBUNGE MATHAYO ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA TIMU YA KATA YA RWAMLIMI...

MBUNGE MATHAYO ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA TIMU YA KATA YA RWAMLIMI KUFUATIA KIFO CHA MCHEZAJI WAKE

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini, Vedastus Mathayo ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mchezaji Angelo Malima.

Mchezaji huyo alikuwa akiichezea timu ya Kata ya Rwamlimi iliyokuwa ikishiriki mashindano ya Mathayo Cup yanayoendelea mjini Musoma na kutolewa hatua za awali.

Angelo alifikwa na mauti usiku wa kuamkia jana kwa tukio la kuchomwa kisu na kupelekea kifo chake.

Àkizungumza na Mzawa Blog kwa njia ya simu amesema.amepokea kwa masikitiko makubwa kufuatia kifo cha mchezaji huyo.

Amesema Angelo alikuwa mchezaji kiongozi wa timu ya Kata ya Rwamlimi na bado alikuwa akitumainiwa na timu yake na taifa kwa ujumla.

Mathayo amesema katika kipindi hiki kigumu anatoa pole kwa familia,timu ya Rwamlimi na wachezaji wote wanaoshiriki mashindano ya Mathayo Cup

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mchezaji wa timu ya Rwamlimi Angelo Malima kilichotokea usiku wa kuamkia jana”

“Natoa pole kwa familia ya marehemu,timu ya Kata ya Rwamlimi na wachezaji wote na mashabiki wanaofatilia mashindano ya Mathayo Cup aliyokuws akishiriki mashindano hayo” amesema .Mathayo.

Mchezaji huyo amewahi pia kuichezea timu ya Biashara United katika msimj wa 2020 na 2021 huku wachezaji aliocheza nao wakimzungimzia kuwa alikuwa ni mchezaji mwenye nidhamu kubwa nje na ndani ya uwanja..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!