Home Kitaifa MBUNGE MATHAYO ATIMIZA AHADI YAKE KWA MKUU WA KIKOSI CHA FFU MUSOMA...

MBUNGE MATHAYO ATIMIZA AHADI YAKE KWA MKUU WA KIKOSI CHA FFU MUSOMA YA KUKARABATI GARI YA POLISI

Na Shomari Binda-.Musoma

MBUNGE jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo ametimiza ahadi yake kwa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU mkoa wa Mara) ya kukarabati fari kwaajili ya kusaidia usafiri.

Ahadi alitoa ahadi hiyo ya shilingi milioni moja (1,000,000) aliitoa baada ya kuombwa wakati akiwa mgeni rasmi kwenye ufungaji wa mafunzo ya askari wakaguzi mkoa wa Mara yaliyofanyika septemba 27.

Kiasi hicho Cha fedha kimekabidhiwa leo 20/10/2023 na katibu wa mbunge hiyo Christopher Majala kwa niaba ya mbunge wa Jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo.

Majala amesema.mbunge aliahidi na ametekeleza ahadi yake kwa wakati ili kuwasaidia askari kutimiza majukumu yao.

Amesema mbunge ameahidi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi ili kupambana na uhalifu na wahalifu jimbo la Musoma mjini liendelee kuwa salama.

Akipokea kiasi hicho cha fedha kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Mara na askari,mkuu wa kikosi hicho Cha kutuliza ghasia ASP Edwin Simon amemshukuru mbunge Mathayo kwa kutimiza ahadi yake hiyo kwao.

Amesema sasa wanaenda kukarabati gari hiyo ili iweze kusaidia usafiri kwa ajili ya kusambaza askari wanaoenda kutimiza majukumu yao.

Mkuu huyo wa kikosi amesema gari hilo litawasaidia hasa wakati huu wa mvua zinazoendelea kunyesha Musoma mjini na mkoa wa Mara kwa ujumla_

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!