Home Kitaifa MBUNGE MATHAYO APIGIA CHAPUO BANDARI YA MUSOMA KUFUFULIWA

MBUNGE MATHAYO APIGIA CHAPUO BANDARI YA MUSOMA KUFUFULIWA

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema bandari ya Musoma ikifufuliwa itainua uchumi wa vijana wa Kata ya Iringo na taifa kwa ujumla.

Hayo ameyasema kwenye mkutano wake wa pili wa hadhara kwenye uliofanyika Kata ya Iringo katika muendelezo wa kutembelea Kata 16 za jimbo la Musoma mjini.

Amesema katika kipindi cha nyuma vijana wa Kata ya Iringo na kutoka maeneo mengine walikuwa wakitegemea bandari hiyo tofauti na sasa.

Mathayo amesema wapo watu wanaopotosha kuhusiana na masuala ya bandari hususani uwekezaji unaokwenda kufanyika bandari ya Dar es salam na kuwachanganya wananchi

Amesema wakati kamati ikiendelea na suala la bandari ya Dar es salaam na kuwaomba kuitembelea pia bandari ya Musoma kwaajili ya kuifufua na kuibua ajira

“Hapa Iringo tuna bandari yetu hii ikifufuliwa itainua uchumi wa vijana wetu na kufanya mifuko kutuna na kunufaika”

“Hakuna Bandari inayouzwa kama wapotoshaji wanavyosema huko mitaani na hata hii bandari yetu itakuja kutunufaisha”

Mathayo amesema bado ataendelea kushirikiana na wananchi wa jimbo la Musoma mjini kama ambavyo wamekuwa wakimpa ushirikiano.

Meya wa halmashauri ya manispaa ya Musoma Patrick Gumbo amesema utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM katika jimbo la Musoma mjini inaendelea kutekelezwa vizuri kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo

Diwani wa Kata ya Iringo Juma Hamis (Igwe) amemshukuru mbunge Mathayo kwa kazi anayoifanya ikiwemo kuwawezesha vijana kiuchumi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!