Home Kitaifa MBUNGE MATHAYO AMFIKISHIA KINANA CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA VIWANDA MUSOMA

MBUNGE MATHAYO AMFIKISHIA KINANA CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA VIWANDA MUSOMA

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amemfikishia kilio cha ukosefu wa viwanda katika mji wa Musoma Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulhaman Kinana na kupelekea uchumi kuwa chini.

Kilio hicho amekitoa kwenye kikao kilichowashirikisha viongozi na wanachama wa CCM Musoma mjini na Makamu Mwenyekiti huyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa chama hicho mkoa wa Mara.

Amesema utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika jimbo la Musoma mjini imetekelezwa vizuri sekta mbalimbali na kikwazo imekuwa masuala ya kiuchumi.

Mathayo amesema miradi ya maji,elimu,afya na hata miundombinu imetekelezwa na jambo la ukosefu wa viwanda imekuwa changamoto.

Amesema chama kama ambavyo kina isimamia serikali ni muda wa kuhakikisha mkoa wa Mara unatazamwa kwenye eneo la viwanda.

Tunakukaribisha sana Musoma mjini ilani ya uchaguzi imetekelezwa vizuri lakini tunayo changamoto ya ukosefu wa viwanda.

Tukiwa na viwanda hali ya uchumi itaimarika na siasa ndani ya Musoma mjini itaendelea kuwa nzuri na CCM itaendelea kushinda kwenye kila uchaguzi”, amesema

Akizungumza kwenye kikao hicho Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulhaman Kinana alianza kukemea suala la viongozi ngazi ya wilaya ya Musoma mjini kusigana na kuleta kutoelewana ndani ya chama.

Amesema wanachama wapo salama na wanakipenda chama chao tatizo limekuwa kwa viongozi wa ngazi ya juu.

Kinana amesema ufatiliaji wa siasa za Musoma mjini ameuachia uongozi wa mkoa kushighulikia ili lisiweze kufika ngazi ya rufaa ya taifa.

Amesema katika masuala ya maendeleo mji wa Musoma umekuwa na mabadiliko makubwa na kuwapongeza viongozi wa chama na serikali

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!