Home Kitaifa MBUNGE MATHAYO AKABIDHI NG’OMBE,MIPIRA NA FEDHA MASHINDANO POLISI JAMII CUP MUSOMA

MBUNGE MATHAYO AKABIDHI NG’OMBE,MIPIRA NA FEDHA MASHINDANO POLISI JAMII CUP MUSOMA

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo leo agosti 15 amekabidhi ng’ombe, mipira 16 na fedha kiasi cha shilingi laki 2 kwaajili ya mashindano Mathayo Polisi Jamii Cup 2024.

Ng’ombe,mipira na fedha imekabidhiwa kwa mkuu wa polisi wilaya ya Musoma kama sehemu ya zawadi kwenye mashindsno hayo yanayoyarajiwa kuanza hivi karibuni kwa kushirikisha timu Kutoka Kata 16 za manispaa ya Musoma.

Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya mbunge huyo Meya wa manispaa ya Musoma Patrick Gumbo amesema huu ni mwaka wa pili anadhamini mashindano hayo kwa lengo la kuwaweka vijana pamoja na kuinua viwango vyao.

Amesema mbunge Mathayo ni mwanamichezo ambaye baada ya kuombwa na jeshi la polisi wilaya ya Musoma kuwa sehemu ya kufanikisha mashindano hayo hakusita.

” Mheshimiwa mbunge ameenda kwenye vikao vya bunge na ameniagiza nikabidhi mipira na ng’ombe kama zawadi kwenye mashindano ya Mathayo Polisi Jamii Cup.

” Ng’ombe itakuwa zawadi ya bingwa wa mashindano na mshindi wa pili atapata zawadi ya fedha kiasi cha shilingi laki 2 ambazo pia zitatolewa na Mheshimiwa mbunge “,amesema Gumbo.

Akipokea zawadi hizo kwa niaba ya mkuu wa polisi Wilaya ya Musoma Mrakibu Msaidizi wa Polisi( ASP)Magengeli Ntinginya amemshukuru mbunge wa jimbo la Musoma mjini kwa zawadi alizozitoa kwaajili ya mashindano hayo.

Amesema madhindano lengo la mashindano ya Polisi Jamii Cup ni kuwaweka vijana pamoja kupitia michezo na kuwapa elimu ya kuzuia uhalifu na kutoa taarifa za wahalifu.

Ntinginya amesema Mathayo amekuwa mdau mkubwa wa mashindano hayo katika kuyafanikisha na kuwaomba wadau wengine kuchangia ili kuweza kufanikisha kwa ufanisi zaidi

” Tunamshukuru sana mbunge Mathayo kwa hiki alichokitoa na tunawaomba wadau wengine watushike mkono ili tufanikishe zaidi mashindano haya ambayo tunatarajia kuanza hivi karibuni “,amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!