Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini, Vedastus Mathayo ameshuhudia timu ya Mwigobero fc ikitinga fainali ya mashindano ya Mathayo Cup 2023.
Katika nusu fainali hiyo timu ya Mwigobeto imeifungasha virago timu ya Makoko fc kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3-2 baada ya dakika 90 kumalizika kwa pacha ya 0-0
Kwa kuingia fainali hiyo timu ya Mwigobeto itacheza na Nyamatare fc kwenye mchezo wa fainali ya mashindano hayo.
Akizungumza uwanjani hapo na mashabiki wsliohudhuria mchezo huo,mbunge wa jimbo la Musoma mjini ambaye ndiye muandaji wa mashindano hayo amesema baada ya kumalizika kwa mashindano haya yanaanza mashindano mengine.
Amesema siku ya jumatatu kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa 3 kati ya Makoko na Nyakato ataweka wazi zawadi za washindi watakazopata siku ya fainali.
“Nimefurahia mwenendo wa mashindano na furaha waliyonayo mashabiki nawaahidi kufanya bandika bandua ya mashindano”
“Lakini pia siku ya jumatatu kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ntawaambia zawadi watakazopata washindi” amesema Mathayo.
Diwani wa Kata ya Mwigobeto Marian Sospeter amewapongeza wachezaji wake kwa kupambana na kuingia fainali.
Amesema wengi walikuwa wakiibeza timu yake lakini imewashangaza na wanakwenda kujipanga kuchukua ubingwa.