Home Kitaifa MBUNGE MATHAYO AIOMBA SERIKALI KUPELEKA FEDHA KWENYE MASOKO MUSOMA

MBUNGE MATHAYO AIOMBA SERIKALI KUPELEKA FEDHA KWENYE MASOKO MUSOMA

Na Shomari Binda

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini, Vedastus Mathayo, kuona utarstibu wa kufikisha fedha kwenye masoko ili kuwawezesha wajasiliamali na wananchi kiuchumi.

Kauli hiyo ameitoa bungeni wakati akichangia kwenye Wizara ya Fedha wakati wa mjadala wa wizara hiyo kwenye bunge la bajeti linaloendelea.

Amesema serikali katika jimbo la Musoma mjini imefanya mambo mengi ya kijamii ikiwemo afya, elimu, maji na miundombinu kilichobaki ni uchumi wa wananchi.

Mathayo amesema jimbo la Musoma mjini inayo masoko ya Mwigobero, soko kuu, Nyasho na soko la saa nane ambayo wajasiliamali wake wanahitaji kuwezeshwa kiuchumi.

Amesema mikopo inayotolewa kupitia taasisi za kifedha imekuwa na changamoto ya upatikanaji wake lakini serikali ikiwezesha kupitia kwenye masoko itawasaidia.

Mbunge huyo amesema wakati serikali ikiendelea kuangalia utaratibu mzuri wa mikopo ya asilimia 10 inaweza kupeleka fedha kwenye masoko wakajikopesha.

Licha ya serikali kupeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika jimbo la Musoma mjini sasa wananchi wanahitaji fedha mfukoni” amesema Mathayo.

Aidha Mathayo ameishukuru serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,kwa kuendelea kuliona jimbo la Musoma mjini kwa kutoa fedha za miradi ya jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!