Home Kitaifa MBUNGE MATHAYO AHAIDI UMEME WA ELFU 27 KWA WANANCHI MTAA WA BWERI...

MBUNGE MATHAYO AHAIDI UMEME WA ELFU 27 KWA WANANCHI MTAA WA BWERI BUKOBA

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amewahakikishia wananchi wa mtaa wa Bweri Bukoba kupata umeme wa gharama nafuu.

Amesema umeme huo wananchi wataupata kwa gharama ya shilingi elfu ishilini na saba (27,000,) na kuwataka kujiandaa kuingiza majumbani.

Kauli hiyo ameitoa kwenye mkutano wa hadhara na wananchi hao liofanyika kwenye shule ya msingi Bweri Bukoba.

Amesema mkandarasi tayari ameshapatikana kwaajili ya mradi wa umeme wa Rea ambao unakuja kuwanufaisha wananchi.

Mathayo amesema awali alishamfikisha eneo hilo aliyekuwa Waziri wa Nishati aliyepita na kufanya uzinduzi wa awali ambao ulisimama awali.

Amesema awamu hii kila mwananchi anayehitaji kuunganishiwa umeme ajiandae na utamfikia nyumbani kwake.

Leo nimekuja kuwasikiliza wananchi wa Bweri Bukoba lakini najua hapa ipo changamoto ya umeme niwahakikishie Rea inakuja na mkandarasi ameshapatikana.

Naomba tujiandae kwa hilo na mambo mengine mazuri ya miradi mbalimbali yanakuja ikiwa ni pamoja na maji,afya na elimu shule mpya 2 zimejengwa”,amesema Mathayo.

Amesema wakati wote amekuwa akiumiza kichwa namna ya kuwasaidia wananchi wa mtaa wa Bweri Bukoba kwaajili ya kusukuma mbele maendeleo.

Mbunge huyo amesema wananchi wa mtaa wa Bweri Bukoba wanapaswa kushukuru kwa maendeleo yaliyopo wakati serikali ikiendelea kuleta fedha nyingi kwaajili ya miradi ya maendeleo.

Wakizungumza kwenye mkutano huo wananchi wa mtaa wa Bweri Bukoba wamemshukuru mbunge huyo kwa jitihada mbalimbali za kuwaletea maendeleo.

Wamesema ujenzi wa shule 2 za msingi na sekondari zimepatikana hivyo maendeleo mengine yatafikiwa na miradi ya maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!