Home Kitaifa MBUNGE IDDI AWATAKA WAUMINI WA KISLAMU KUWA WAMOJA NA KUWA NA MSHIKAMANO.

MBUNGE IDDI AWATAKA WAUMINI WA KISLAMU KUWA WAMOJA NA KUWA NA MSHIKAMANO.

Na Joel Maduka, Msalala.

Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim Iddi,amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kuwa wamoja na kushikamana kwa nia ya kudumisha amani ndani ya Dini hiyo akiimiza pia kwa waumini wa dini hiyo kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kujiinua kiuchumi.

Mbunge Iddi amesema hayo mapema leo tar 8 October 2023 ,wakati akiwa ni mngeni Rasmi kwenye Maulidi ya Kiwilaya iliyofanyika Kijiji cha Kakola Kata ya Bulyanhulu.

Amesema ni vyema kwa waislamu wakaangalia namna njema ya kufuata misingi ya namna gani wanaweza kuimalisha uchumi wao ambao utawainua na kuwasaidia na kuachana na migogori inayo warudisha nyuma kimaendeleo.

Kwenye suala la elimu shule nyingi tulizozianzisha waislamu zimekuwa na migogoro kiasi kwamba aziwezi kuendelea mbele kutokana na kuwajawa na fitina ambazo zinaturudisha nyuma naomba tuhishi katika kauli mbiu ya mufti wetu ambayo inasisitiza waislamu kuwa na uchumi imara“Iddi Kassim Iddi Mbunge Jimbo la Msalala.

Niwaombe ndugu zangu waislamu tuaminiane tuweze kuupeleka uslamu mbele zaidi dini yetu iwe ni ya kutangaza amani na sio migogoro isiyokuwa na umuhimu tunaitaji tuwe wamoja tupendane tusaidiane kwani mtu wetu Mohamed alisisitiza suala la umoja“Iddi Kassim Iddi Mbunge Jimbo la Msalala.

Sanjali na Hayo Mbunge Iddi amechangia kiasi cha Sh,Milioni mbili kwaajili ya kumalizia ujenzi wa maduka ya Msikiti wa Ijumaa Kakola.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!