Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ujenzi wa zahanati ya Kata ya Mkoma wilayani Rorya.
Ukamilishwaji wa ujenzi wa zahanati hiyo unakuja ili kusaidia wananchi wa Kata hiyo kuweza kupata huduma za afya karibu na maeneo wanayoishi.
Akizungumza na Mzawa Blog diwani wa Kata ya Mkoma Ayoi Musa amesema wamemualika mbunge huyo kuwa mgeni rasmi kutokana na moyo wake wa kuchangia na kuhamasisha shughuli za maendeleo.
Amesema mbunge Ghati kwenye kuchangia maendeleo yupo mstari wa mbele na kudai uwepo wake utasaidia kupata vifaa na fedha kwaajili ya ukamilishaji.
Ayoi amesema huduma za afya ni suala la msingi na wananchi walianza kwa kujitoa nguvu kazi na michango ili kuweza kupata zahanati kwenye Kata yao.
Amesema Kata hiyo ya Mkoma kwa sasa haina zahanati ya kupata huduma za afya na wamekusudia kuipata na baadae serikali iweze kuwapatia wahudumu.
“Tumeamua kumualika mheshimiwa Ghati kwenye harambee ya ukamilishaji wa zahanati ya Kata yetu tukiamini ni mtu sahihi katika kujitoa katika kuchangia shugjuli za maendeleo.“
” Harambee hii itafanyikia Obwere Shirati desemba 6 na licha ya mbunge Ghati tumealika pia wageni mbalimbali ili waweze kufika na kuweza kufika na kuweza kutuchangia ili kuweza kukamilisha ujenzi wa zahanati”,amesema Ayoi.
Kwa upande wao wananchi wa Kata ya Mkoma wamesema wapo tayari kuwapokea wageni watakaofika kwenye harambee hiyo na kushirikiana nao ili kuweza kupata zahanati.