Home Kitaifa MBUNGE GHATI CHOMETE AKABIDHI TOFALI 1000 UJENZI NYUMBA YA KATIBU UWT WILAYA...

MBUNGE GHATI CHOMETE AKABIDHI TOFALI 1000 UJENZI NYUMBA YA KATIBU UWT WILAYA YA SERENGETI

Na Shomari Binda-Serengeti

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara, Ghati Chomete amekabidhi tofali 1000 kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT wilaya ya Serengeti.

Huu ni muendelezo wa mbunge huyo kuchangia ujenzi wa nyumba za watumishi wa UWT katika wilaya za mkoa wa Mara ambapo.hivi karibuni aliachangia mifuko ya saruji na kuanzisha ujenzi wa msingi wa nyumba ya Katibu wa UWT wilaya ya Musoma mjini.

Akikabidhi tofali hizo wilayani Serengeti katika tukio lililohudhuliwa na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na madiwani kwa niaba yake, diwani wa Kata ya Mwigobero, Mariam Sospeter amesema suala la makazi bora ni muhimu na mbunge ameguswa na kuchangia.

Amesema mbunge Ghati bado yupo kwenye majukumu na kumuagiza kupeleka tofali hizo ili kuendeleza ujenzi huo.

Mariam amesema mbunge huyo amekuwa akichangia maeneo mbalimbali na kwa sasa ameamua kuchangia nyumba ya Katibu wa UWT wilaya ya Serengeti.

Amesema Katibu kama mtumishi anapopata makazi mazuri ambayo hayana usumbufu anapata fursa ya kutekeleza majukumu yake vizuri.

Mheshimiwa mbunge Ghati Chomete bado yupo kwenye majukumu ya kibunge na ameniagiza kuleta mchango wake”

“Naomba mpokee mchango wake wa tofali 1000 ili ujenzi uweze kuendelea lakini ameahidi kuendelea kuchangia pale atakapopata nafasi” amesema Mariam.

Kwa upande wao madiwani wa viti maaalum waliokuwepo kwenye makabidhiano hayo wamemshukuru mbunge Ghati kwa moyo wake wa kujitolea katika kuchangia masuala mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!