Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa viti maalum Ester Bulaya amesema anayo furaha na kujivunia mashindano ya Bulaya Cup kutoa wachezaji wengi tangu yalipoanzishwa.
Kauli hiyo aeitoa kwenye uwanja wa sabasaba mjini Bunda wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Bulaya Cup 2023.
Amesema Bulaya Cup imefanyika kwa mafanikio tangu kuanza kufanyika kwa kuwa wapo wachezaji ambao wanazichezea timu kubwa waliopitia mashindano hayo.
Bulaya ambaye ameshuhudia mchezo wa ufunguzi kati ya timu ya Bunda Queen na Bunda Girls michezo ambao Bunda Queen wameshinda mabao 2-0 amesema watu wa Bunda wanayafurahia mashindano hayo na sasa yamekuja na nguvu kubwa.
Amesema kwa kipindi hiki cha mashindano ya mwaka huu watawapa fursa pia wachezaji wenye ulemavu kuonyesha vipaji vyao pamoja na.michezo mingine.
” Mashindano yetu yamekuwa na mafanikio makubwa tangu kuanza kufanyika na sasa yamerejea tena kwa kasi ile ile.
” Safari hii tutashirikisha michezo mbalimbali ili kutambua vipaji vingi zaidi na kuwezesha kwenda timu kubwa kama walivyofanya watangulizi waliopita”,amesema Bulaya.
Baadhi ya wadau walioshiriki ufunguzi huo wamempongeza mbunge Ester Bulaya kurejesha mashindano hayo ambayo yamekuwa na mafanikio kwa kuibua vipaji.
Jumla ya timu 20 za soka zinashiriki mashindano ya Bulaya Cup 2023 pamoja na mchezo wa mpira wa pete.