MBUNGE wa Vijana Ng’washi Kamani amewataka Wanafunzi wa kike kujitunza ili waweze kufikia malengo yao ya baadaye waliyojiwekea.
Wito huo ameutoa leo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Nganza iliyopo jijini Mwanza alipokuwa akizungumza na Wanafunzi wa Kidato Cha Sita.
Aliwambia kuwa wanao wajibu wa kujifunza kwa kuangalia Wanawake Viongozi kwenye Taifa la Tanzania wakianza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Jenister John ambaye ni miongoni mwa Wanafunzi wa Kidato Cha Sita kwenye Shule hiyo alimpongeza Mbunge huyo kijana kwa kudhubutu na hivyo kuweza kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.