Na Shomari Binda
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara Agness Marwa ameendelea kutekeleza ahadi yake ya kuwafikisha viongozi wa UWT mkoa wa Mara visiwani Zanzibar.
Huu ni muendelezo wa ziara iliyopewa jina la ” Mara To Zanzibar Royal Tour”insyodhaminiwa na mbunge huyo kwa viongozi wa wilaya zote za mkoa wa Mara.
Safari hii ziara hiyo imewahusisha viongozi wa UWT kutoka Musoma mjini na madiwani wa viti maalum wilaya ya Bunda.
Viongozi hao wametembelea shule ya msingi Kizimkazi ambayo amesoma elimu ya msingi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Licha ya kutembelea shule hiyo viongozi hao pia wametembelea maeneo mbalimbali ikiwemo ofisi za CCM tai la Kizimkazi.
Akizungumza na Mzawa Blog mbunge huyo amesema lengo la ziara hiyo no kumuunga mkono Rais Samia kwa kutangaza utalii wa ndani.
Amesema hiyo ni ahadi yake aliyowapa viongozi hao wa UWT kutoka wilaya zote za mkoa wa Mara na tayari wilaya nyingine wameshafika visiwani humo.
Mbunge hiyo amesema kupitia ziara hiyo viongozi hao wamekuwa wakijifunza mambo mbalimbali yakiwemo ya kisiasa
Baafhi ya viongozi walioshirii ziara hiyo wamemshukuru mbunge huyo na kudai wamejifunza mengi kupitia ziara hiyo aliyoiratibu.