Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Mara,Agnes Marwa,amewawezesha vifaa mbalimbali wanawake na vijana ili kutimiza majukumu yao.
Vifaa hivyo yakiwemo majiko ya gesi,mifuko ya saruji,vifaa vya michezo na taulo za like vimetolewa na mbunge huyo kwa nyakati tpfauti kwenye Kata ya Mugango na Bulinga.
Akiwa kwenye mkutano wa hadhara Kata ya Mugango alikabidhi majiko ya gesi kwa wanawake wakiwemo wajasiliamali wa biashara ya mgahawa.
Akikabidhi majiko hayo,mbunge Agnes amesema ni jambo jema kuwawezesha wanawake ili kuweza kukabiliana na changamoto za maisha.
Amesema ukimuwezesha mwanamke japo kwa kidogo anakitumia vizuri na kussifia familia nzima kwa kuwa ndio muangalizi wa karibu
Licha ya kusaidia majiko hayo ya gesi lakini amewasaidia pia vifaa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kwaajili ya kuvaa na kuonekana hasa nyakati za usiku.
Akiwa Kata hiyo ya Mugango ametoa vifaa vya michezo kwa vijana ili kuweza kuinua viwango vyao na kujiajili kupitia michezo.
Mbunge Agnes akiwa eneo la Bulinga ametoa mifuko ya saruji kwaajili ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Bulinga ili wanafunzi wajifunze kwa vitendo masomo ya sayansi.
Aidha amekabidhi kwa wanafunzi 200 taulo za kike shuleni hapo na kuahidi kuendelea kuwasaidia wanafunzi wa kike ili wasome kwa amani.