Home Kitaifa MAZOEZI NI AFYA  GEITA JOGGING CLUB YAJIPANGA KUKUZA USHIRIKI WA JAMII

MAZOEZI NI AFYA  GEITA JOGGING CLUB YAJIPANGA KUKUZA USHIRIKI WA JAMII

Klabu ya mazoezi ya Geita Jogging, yenye makao yake Manispaa ya Geita, imehitimisha mwaka 2024 kwa sherehe maalum za kupongezana na kuandaa mikakati ya mwaka 2025. Lengo la klabu hiyo ni kuimarisha ushiriki wa wananchi katika mazoezi, ili kujenga jamii yenye afya bora.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa klabu, Vallence Ibarahimu, alisema kuwa mwaka 2025 wanatarajia kuongeza idadi ya wananchi wanaojiunga na klabu kwa ajili ya kufanya mazoezi. Alisisitiza kuwa mazoezi ni moja ya njia bora za kujikinga na maradhi mbalimbali.

Kwa upande wake, Afisa Habari wa klabu hiyo, Ruhasha Nyogwa, alielezea mafanikio aliyoyapata kupitia klabu, ikiwemo kuboresha afya yake na kupata marafiki wapya waliomsaidia katika mambo mbalimbali ya kijamii.

Aidha, Afisa Michezo wa Mkoa wa Geita, Rojas Bahati, alisema kuwa serikali ya mkoa inatambua umuhimu wa klabu za mazoezi katika kuhamasisha afya kwa wananchi. Aliahidi kuendelea kushirikiana na Geita Jogging Club kuhakikisha wanawafikia wananchi wengi zaidi ndani ya mkoa huo, kwa lengo la kuwahamasisha kuzingatia mazoezi kama sehemu ya maisha yao ya kila siku.Shughuli hiyo ya kufunga mwaka imeacha alama kwa wanachama wa Geita Jogging Club na jamii kwa ujumla, ikiwa ni njia ya kuimarisha mshikamano na kusisitiza umuhimu wa afya bora kupitia mazoezi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!