Mawe makubwa mawili ya Tanzanite moja likiwa na uzito wa kilo 3.74 na jingine likiwa na uzito wa kilo 1.48 yamepatikana ndani ya machimbo ya Tanzanite Mirerani kutoka kwa mchimbaji mdogo, Anselm J. Kawishe. Mawe hayo yanatarajiwa kununuliwa na Serikali kwa shilingi 2,245,571,543.46