Home Biashara MAVUNDE APONGEZA UWEKEZAJI MAABARA YA MSA GEITA

MAVUNDE APONGEZA UWEKEZAJI MAABARA YA MSA GEITA

  • Inapima Sampuli za Madini kwa Mionzi (PhotoAssay)
  • Inatoa majibu ndani ya masaa mawili
  • Asilimia 99.8 ya Wafanyakazi ni Watanzania

Zaidi ya Shilingi Bilioni 5 zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS inayomiliki Maabara ya upimaji wa sampuli za Madini kwa kiwango cha kimataifa mkoani Geita.

Hayo yamebainishwa Septemba 27 , 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MSALABS Mugisha Lwekoramu wakati wa ufunguzi wa Maabara hiyo.

Akizungumzia kuhusu teknolojia inayotumika katika Maabara hiyo Lweramu amesema Maabara inatumia teknolojia ya kisasa ya upimaji wa sampuli kwa njia ya mionzi yaani (PhotoAssay) ambayo ni rafiki kwa utunzaji mazingira kwasababu haitumii kemikali au moto katika upimaji sampuli.

Akielezea kuhusu ufanisi wa teknolojia hiyo , Lwekoramu amesema ni sehemu ya mapinduzi ya teknolojia kwasababu inamwezesha mdau kupata majibu ya sampuli ndani ya masaa mawili ni tofauti ukilinganisha na teknolojia ya zamani ya kutumia moto na kemikali.

Kwa upande , wake Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Maabara hiyo kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya madini , akiwataka kuendelea kufungua matawi mengine nchini.

Aidha , amewapongeza pia kwa kuweza kuajiri watanzania kwa asilimia 99.8 akiamini kuwa wafanyakazi hao wataendelea kujifunza utumiaji wa teknolojia hiyo na kutoa ujuzi huo kwa watanzania wengine.

Mhe .Mavunde, ameahidi kuwa Serikali awamu ya sita itaendelea kuwatengenezea mazigira rafiki ya uwekezaji na kutoa ushirikiano kwa jinsi itakavyohitajika katika mnyororo mzima wa sekta

Awali , Mhe .Mavunde alitembelea kampuni ya Blue Coast inayotoa huduma migodini kama vile Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) kwa lengo la kuangalia maendeleo ya uwekezaji.

Katika shughuli hizo , Mhe.Waziri aliambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Madini,Mkuu wa Mkoa Geita , Mkuu wa Wilaya ya Chunya , Mtendaji Mkuu wa GST na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!